Jumapili, 9 Februari 2014

Njia Mpya ya Kuuza Bidhaa za Makampuni ya Network Marketing


Umewahi kusikia makampuni kama Forever Living Products, GNLD, Amway, Empower Network, DSDomination n.k ambayo huuza bidhaa zake kwa njia y mtandao yaani Network Marketing. Makampuni ambayo ni maarufu hapa Tanzania ni Forever Living na GNLD. Makampuni haya huuza bidhaa zitokanazo na mimea na huuza kwa njia ya mtandao (Network).

Network Marketing ni njia ya kuuza bidhaa ambayo imekuwapo tangiu miaka mingi. Biashara ya network inataka mtu ajiunge kwenye kampuni na kununua bidhaa za kuanzia. Mara nyingi inatakiwa bidhaa hizo uzitumie kwanza na zingine uziuze. Kutumia bidhaa hizo inakupa uelewa wa jinsi zilivyo nzuri na zinavyosaidia matatizo ya watu. Baada ya kuziuza na kutumia unatakiwa uanze kutafuta watu ambao watajiunga na kampuni na wao kuanza kuuza bidhaa hizo. 

Kwa kila mtu anayejiunga, aliyemuingiza hupata kamisheni na bidhaa atakayouza utapata pasenti fulani ya mauzo hayo. Chukulia kwa mfano, umeingiza watu watano, kila uliyemuingiza utapata kamisheni, na kila bidhaa itakayouzwa na watuwako uliowaingiza utapata pasenti ya mauzo hayo. Ndiyo maana inaitwa biashara mtandao.

Faida kubwa ya  kujiunga n makampuni haya ni kuwa mtu anakuwa na biashara yake na kisha anaweza kuifanya akiwa nyumbani kwake bila kukutana na bosi wala foleni za kila siku za mjini. Anajipangia muda wa kufanya kazi na muda wa kupumzika. 

Kampuni hizi zilivyoingia nchini zilipokelewa vizuri sana na watu walianza kutumia bidhaa zake sambamba na kujiunga kama wasambazaji. Hata hivyo biashara hizi zimeendelea kupungua umaarufu wake. Tumefanya utafiti wa haraka kwa nini watu hawajiungi sana na makampuni haya.


 Sababu ambazo watu wengi wanatoa ni kuwa hawezi kutembeza biashara kutoka nyumba hadi nyumba, au maofisini kutafuta wateja. Pia kuna hii mikutano y majumbani ya kualika ndugu na marafiki na kuwaelezea biashara, inaonekana kutowafurahish walio wengi.  Kwa ujumla njia zinazotumika kuuza na kuingiza wasambazaji ndiyo hasa zimeshusha hamasa ya walio wengi kujiunga.

Kwa kuzingatia sababu hizi, sisi JCM Marketing Coach tumebuni njia rahisi ya nyepesi ya kuuza na kuhamisisha waliowengi kujiung kama wasambaji. Njia hizi hazihitaji upigie watu 100 simu kila wakati, hakuna tena kuzunguka maofisi na kubembeleza watu wanunue bidhaa zako, hakuna mikutano ya majumbani na mahoteli tena. 

Kama unataka kujiunga na biashara hizi n kujifunza mbinu mpya za kuuza bidhaa hizi tafadhali wasiliana nasi. Pia usiache kutoa maoni yako hapo chini.

Pata Bidhaa za Aloevera ili Kufurahia Maisha Yako


  • Kwa mahitaji yoyote ya bidhaa hizi za afya na usafi,
  • Kwa ushauri wa matumizi ya bidhaa hizi,
  • Kwa ushauri wa magonjwa yanayotibiwa na bidhaa hizi za Aloevera;
  • Kwa ushauri jinsi ya  kuwa msambazaji wa bidhaa hizi na kutajirika;
PIGA SIMU NA. 0655500707 au 0717342020





6




Jumamosi, 10 Novemba 2012

Kutokuwa Wabunifu ni Madhara ya Kufikiria Kijamaa?



Kumekuwa na mijadala mingi sana kuhusu watanzania wengi kutokuwa wabunifu ukulinganisha na nchi zingine majirani. Ukichukulia mfano wa Kenya, wakenya wamekuwa na biashara nyingi sana hapa kwetu ukilinganisha na zila za watanazania. Ukiangalia katika hali ya ubunifu na ujasiriamali kwa ujumla Kenya wanaonekana wako mbele sana ukilinganisha na sisi. Hata bidhaa zinazoingia Tanzania kutoka Kenya ni nyingi sana ukilinganisha na za watanzania zinazoenda Kenya.

Hivi ni kweli kuwa kutokuwa wabunifu kulisababishwa na fikira za kijamaa?
Kwa tafsiri rahisi ujamaa ni umilikaji wa njia za uchumi kwa pamoja. Wakati wa ujamaa mashirika yote ya umma yalimilikiwa na watanzania kwa pamoja. Mashirika kama RTC, UDA, NBC, NIC National Milling, n.k.yalimilikiwa na umma. Ilitegemewa mashirika haya yafanye biashara kisha yagawe gawio kwa serikali ili serikali nayo itoe huduma bure kwa wananchi. Hapa ndiyo dhana halisi ya ujamaa na umilikaji wa mitaji kwa pamoja ilipokuwa imejitika. Hivyo wananchi walitegemea serikali iwafanyie kazi katika mashirika yake na kuwapa mahitaji yao. Ndiyo maana kulikuwa na maduka ya kaya, mashamba ya pamoja ili uzalishaji uwe wa pamoja na kisha kugawana mazao. 

Bahati mbaya, kwa hapa kwetu dhana ya ujamaa haikuleta matunda yaliyotarajiwa. Mashirika yote yakafa baada ya watu wasiokuwa waaminifu kupewa kusimamia mashirika haya. Wakayafilisi yakaisha kabisa. Badala yake waliokuwa na dhamana ya kusimamia mashirika hayo wakajinufaisha na mashirika hayo mpaka yakashindwa kujiendesha. Itakumbukwa kuwa wakati wa awamu ya tatu utawala,  mashirika mengi yalikuwa yakitegemea ruzuku kutoka serikalini. Sasa badala ya mashirika haya kuilipa serikali gawio, serikali ikawa inayagharimia mashirika haya. Jambo hili halikuwa sawa ndiyo maana serikali ikayabinafsisha ili kuhamisha mizigo huo kwa sekta binafsi. 

Baada ya ubinafsishaji huu ambao ulisukumwa na dhana ya ubepari ulioingia Tanzania kimya kimya, wananchi hawakuambiwa kuwa umilikaji wa njia za uchumi kwa pamoja sasa basi hivyo watu waanze kukuza mitaji yao. Kuwa mitaji ile waliyoiweka katika mashirika ya umma kuanzia mwaka 1967 wakati serikali ilipowanyang'anya watu majumba na mali zingine ili zimilikiwe na serikali sasa imeisha. Kuwa kimya huku kumewafanya watanzania kuendelea kuelewa kuwa bado tuko kwenye ujamaa hivyo kutegemea serikali kufanya kila kitu. Kaulize vijana wale waliokaa vijiweni, stori ni serikali haijafanya hiki na kile. Serikali haitaweza kukufanyia chochote zaidi ya kuweka miundombinu na mazingira safi ya wewe kubuni na kuanzisha biashara yako. 

Katika kuwaelimisha watanzania kuanza kufikiria na kuwa wabunifu, serikali kwa nyakati tofauti ilitoa mbiu mbalimbali ili watu wazinduke. Kwa mfano kila kitu ni ruksa (Rais Mwinyi),  mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe (Rais Mkapa) na ile ya mabilioni ya JK( Rais Kikwete).  Hizi ni jitahada za serikali kusaidia watanzania kufuta kichwani mwao mawazo ya ujamaa na kuanza kukuza mitaji. Umiliki wa pamoja umeshaisha ndiyo maana hata shule hatuendi za aina moja, hospitali n.k. Hata hivyo juhudi hizi hazitoshi.  Urusi inatumia mabilioni ya dola kwa ajili ya kufuta fikira za kijamaa katika akili za warusi ili waweze kuanzisha na kukuza mitaji yao. Hapa kwetu mbiu tu hazitoshi, tufikirie kuwekeza katika kufuta fikira hizi zinazowafanya watanzania washindwe kuwa wabunifu na kuanzisha na kusimamia biashara zao. Lazima tuwekeze katika fikira sahihi kama tunataka watanzania watoke. 

Hali ya ujamaa imewapumbaza wengi  hata wasomi wetu hawawaelezi watanzania kilichotokea hapo katikati na kuanza kuwafundisha jinsi ya kubadili fikira na fahamu zao ili zijielekeze katika kuanzisha biashara na kuacha kuitegemea serikali kwa kila jambo. Hata nchi za wenzetu ambazo ujamaa umeshindwa wanatumia fedha nyingi sana kuwaelimisha wananchi wao kufuta mawazo ya kutegemea serikali na kuanza kukuza mitaji binafisi.

Sisi Elizabethrose Memorial Institute  tumeona kuwa watu kuendelea kutegemea serikali na kushindwa kubuni na kuanzisha biashara zao ni tatizo linalohitaji juhudi nyingi katika kulitatua. Hatuwezi kuiachia serikali ianze kuendesha mafunzo ya kufuta yale tuliyowaaminisha watanzania, na kuwaelimisha nguvu ya ujasiriamali na kufungua ufahamu wao.  Hatuhitaji kuingia katika mtego ule wa kuiachia serikali kila kiti isipokuwa tumeanzisha madarasa ya mafunzo ya ubunifu wa biashara, kusimamia na kuendeleza biashara. 

Alhamisi, 8 Desemba 2011

MIAKA 50 YA UHURU NA MJASIRIAMALI


Tumedhubutu Tumeweza na Tunasonga mbele " ni kaulimbiu ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.  Bado tuna safari ndefu ya kuwawezesha watanzania waliowengi kuweza kujiajiri na kuondoa utegemezi katika kusubiri kuajiriwa. Leo hata wale waliopata fursa ya kwenda shule hata kufikia elimu ya juu wanazunguka na vyeti vyao kutafuta ajira. Wasomi ni wengi ajira chache, wale wasopata bahati ya kwenda shule hata kufikia elimu ya juu ambao  ndio watanzania waliowengi wako kwenye hali mbaya zaidi ya kuweza kuajiriwa au kujiajiri. Katika msimu huu wa soko huria ufahamu na ubunifu wa hali ya juu unahitajika ili watanzania waliowengi waweze kujiajiri na kuwa wajasiriamali wenye mafanikio.

Tangu uhuru wa Tanganyika mfumo wa ujamaa  na kujitegemea ambao kimsingi ulikuwa na malengo mazuri, mitaji ilimilikiwa kwa pamoja, kulikuwa na maduka ya ushirika, vyama vya ushirika, shule za aina moja ili kuweka usawa kwa wote. Kwa upande mwingine mfumo huu ulidumaza fikra za watanzania walio wengi kujijengea utamaduni wa kuweza kumiliki mitaji yao binafsi  ili kuweza kujiajiri na sio kusubiri kuajiriwa.

Leo tunashaherekea miaka 50 ya uhuru  wa Tanganyika, kwa kiasi kidogo “Tumedhubutu Tumeweza na Tunasonga mbele " kumwezesha mtanzania kumiliki mtaji kwani watanzania walio wengi wameweza kuanzisha na kusimamia biashara zao, walio wachache wamekuwa wajasiriamali wakubwa wenye mafanikio hata kuweza kutoa ajira kwa wengine.

Serikali imejitahidi kuhamasisha wanachi kutotegemea zaidi kuajiriwa na badala yake wajiajiri ili kuweza kukabiliana na soko huria. Serikali pia, imetoa fursa mbalimbali ikiwemo kusaidia kifedha, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mstari wa mbele kwa kutoa ‘mabilioni ya JK’  na taasisi mbalimbali  za fedha wamejitahidi kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapa mikopo ili waweze kuendeleza biashara zao. Kutokana na utafiti wetu tuliofanya, bado masharti ya mikopo yameonekana kuwa ni magumu kwa wajasiriamali. Elimu ya ujasiriamali imekuwa inatolewa kwa kiasi kidogo sana.

Kutokana na utafiti tulioufanya katika taasisi yetu ya Elizabethrose Memorial Institute (EMI) kwa  mwaka huu kwa wajasiriamali na watanzania zaidi ya 100, tumegundua kuwa:
·         Mtazamo na ufahamu wa watanzania(mindset) ndio kiini cha watanzania waliowengi kushindwa kujiajiri, hata walioanza biashara(wajasiriamali) wamekwama, wanashindwa kuendeleza biashara zao, wamekata tamaa. Bado tuna kazi kubwa ya kuwawezesha watanzania kwanza kwa kukomboa fikra zao ili kubadili mtazamo(mindset yao) kujua kwamba wanaweza, wajiamini kwakuwa kila kitu kinaanza kama wazo. Tukiweza kuukomboa ufahamu wa mtanzania tutapiga hatua kubwa sana.

·         Nitaanzaje biashara bila mtaji? Nitapata wapi mtaji wakati masharti ya kupata mkopo ni magumu? Nitafanya biashara gani itakayokuwa endelevu? Haya ndio maswali ambayo watanzania wanajiuliza leo ambayo ndiyo yanawafanya washindwe kujiajiri au kuendeleza biashara zao. Ukweli ni kwamba yote yanawezekana wanahitaji kuelekezwa.

·         Wanashindwa kutumia fursa ya mikopo kwa hofu ya kushindwa kulipa riba au marejesho.

·         Wanafanya biashara kwa kuiga na sio kutokana na vipaji vyao hivyo kushindwa kuwa na biashara endelevu

·         Wanatumia vibaya mikopo wanayopewa hivyo kuishia kufilisiwa. Wanachanganya mtaji na matumizi binafsi.

Kutokana na utafiti huu, Serikali  inashauriwa iziwezeshe taasisi zinazotoa mafunzo ya ujasiriamali kwanza kubadilisha mtazamo(mindset) za watanzania waliowengi,  kuwapa elimu na mbinu mbalimbali za kuwa wajasiriamali wenye mafanikio. Ihamasishe masharti nafuu ya mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

Jumatatu, 19 Septemba 2011

Je Unajua Kama Kuna Mbinu za Kutajirika?


Kuna NGUVU ambayo kila kitu kiliumbwa kutoka  kwake, ambacho kwa asili yake inaruhusu, inapitisha na kuujaza uwazi ulioko katika ulimwengu. 

Wazo linalokuwa katika NGUVU hiyo huzalisha kitu ambacho kimefikiriwa katika wazo hilo. 

Mtu anaweza kutengeneza wazo lake na kwa kuliweka katika NGUVU hiyo isiyokuwa na umbo anaweza kusababisha kitu anachokifikiri kutengenezwa. 

Ili kuweza kufanya haya, mtu lazima atoke katika hali ya ushindani na aingie katika hali ya ufahamu wa ubunifu. Bila hivyo hawezi kwenda sambamba na NGUVU hiyo ambayo siku zote ni bunifu na wala haina roho ya ushindani.  

Mtu anaweza kwenda sawa na NGUVU hii kwa kuwa na shukurani ya kweli kwa baraka ambazo amewahi kupata. Shukurani huunganisha ufahamu wa mtu na akili ya NGUVU ili wazo la mtu liweze kupokelewa na NGUVU hiyo.

Mtu anaweza kubaki katika hali ya ubunifu kama tu akijiunganisha na akili ya NGUVU kupitia hisia za ndani na za siku zote za shukurani. 

Mtu anaweza kutengeneza picha ya vitu anavyotaka kuvipata, kuvifanya au unavyotaka kuwa na ni lazima kushikiria picha ya vitu hicho katika mawazo yake na kuwa na shukurani za ndani kwa NGUVU kwamba amepata hitaji lake. Mtu anayetaka kuwa kuwa tajiri lazima atumie muda wake kufikiria ndoto yake na shukurani kuwa amepokea kile anachokitaka.


Umewahi kuona watu wa elimu sawa, mazingira sawa, biashara sawa na kila kitu kiko sawa, lakini mmoja anakuwa tajiri mwingine fukara wa kutupwa? Au umewahi kuona wale waliokuwa na akili sana darasani wanakuwa masikini huku mbumbumbu wa kutupwa anakuwa tajiri? 

Kuna sayansi na njia sahihi za kuwa tajiri. Hizi zikifuatwa kwa usahihi lazima mtu atakuwa tajiri. Haihitaji uwe New York au London au Paris au kokote walikoendelea ndiyo uwe tajiri. Ndiyo maana hata huko kuna masikini wakubwa wakati Tanzania pia kuna mabilionea na masikini. Hata jagwa la sahara pamoja na ukame kuna matajiri pia. Hivyo kuna mbinu za kuwa tajiri.

Hivyo ni jukumu la kila mtu kujifunza mbinu hizi na sayansi ya kupata utajiri. Elizabethrose Memorial Institute imedhamiria kufundisha wajisiriamali njia sahihi za kupata mafanikio BURE. Maana tunaamini ili kufanikiwa lazima usaidie wengi. Wasiliana wasi tukusaidie.

Ijumaa, 16 Septemba 2011

Je Unaweza Kutengeneza Muujiza Wako?

Je unaweza kutengeneza muujiza wako? Si umeshudia matangazo mengi ya miujiza kuanzia makanisani, miskitini hadi kwa waganga wa kienyeji wote wakitangaza miujiza? Je unafahamu miujiza unavyofanyika? Unafahamu mungu wako anavyokutengenezea muujiza wako?  Miujiza hili inaweza kutokea katika imani yoyote.

Tumezungumza kuwa ufahamu(mind) ikilishwa vizuri inaweza ikafanya jambo lolote. Chakula cha ufahamu, kama nilivyosema kwenye makala iliyotangulia, ni mambo chanya (positive) ambayo tunayaingiza kwenye fahamu zetu. Nilikwenda mbali zaidi nikasema hata miujiza mingi huanzia kwenye ufahamu. Mfano mzuri wa muujiza ulioanzia kwenye ufahamu ni ule wa Daudi, mtoto mdogo kumpiga Goliath Jemedari wa vita. Pia nilizungumza jinsi ambavyo watu wametumia vibaya fahamu zao na kusababisha miujiza mibaya katika maisha yao. Kwa mfano kunuia ugonjwa kwa muda mrefu lazima utakujia, kunuia kifo, lazima kitakufika n.k. Leo napenda tuangalie jinsi fahamu zetu zinavyosababisha miujiza kama tukiweza kuzilisha mambo mema. Kama nilivyosema ufahamu (mind) zina sehemu mbili yaani conscious na subconscious. Hizi zina tabia mbili tofauti. Tuziangalie tabia za sehemu hizi mbili tofauti za ufahamu.

1. Conscious Mind
Sehemu hii ya ufahamu hutengenezwa na viungo vile vitano vya fahamu  kama tulivyosoma zamani kwenye sayansi au biologia. Hivi ni macho kwa kuona, pua kwa kunusa, mwili kwa kuhisi, sikio kwa kusikia na ulimi kwa kuonja. Taarifa zote zinazoingia kwenye ufahamu hupitia kwenye ufahamu wa conscious. Tafiti zinaonesha kuwa taarifa zinazoingia kupitia ufahamu huu huchukua sekunde moja hadi mbili kutulia kwenye akili/ufahamu wetu. Ndiyo maana unakuta kwa siku mtu anakuwa na fikra nyingi nyingi zilizoingizwa kwenye ufahamu kupitia viungo hivyo. Kwa kuwa fikra zinazoingia kwenya akili/fahamu zetu kwa mtindo huu hukaa hapo muda mfupi, basi hizi hazitusaidie chochote. Haziwezi kujenga imani wala haziwezi kujenga tabia ya mtu. Hivyo ni vizuri tusiruhusu au kudhubiti vitu ambavyo vinatakiwa kuingia kwenye akili zetu.

2. Subconscious Mind.
Hii ni sehemu ya pili ya jinsi fahamu zetu zinavyofanya kazi. Sehemu hii hupokea taarifa zote kutoka kwenye conscious mind ambazo zimekaa pale kwa muda mrefu. Sehemu hii hutoa matokea yanayolingana na taarifa ilizozipokea, pia ndiyo sehemu hutengeneza tabia zote za binadamu kama taarifa hizo zikikaa hapa muda mrefu. Kwa mfano, kupitia vile viungo vya fahamu, kama taarifa moja ikikaa pale muda mrefu(kufikiria taarifa kwa muda mrefu) basi taarifa hiyo iwe nzuri au mbaya itakutokea tu. Sehemu hii unaweza kujua inavyofanya kazi kama vile mtoto anavyojifunza lugha. Hujifunza kwa kusikia muda mrefu na kurudia rudia. Kama nilivyosema sehemu hii haichagua baya wa zuri, unachoweka ndicho hukuletea. Kama umeweka kwamba kwenu mmelaani na hamuwezi kufanikiwa, au kuwa viongozi au hata kufaulu mitihani basi fahamu hizo zinakusaidia kuamini hivyo. Ufahamu huu pia ukiulisha kufanikiwa na kukiri kuwa jambo fulani uliweza kwa kurudia rudia basi jambo hilo litatoke hivyo.

Kwa hiyo basi ni vizuri tukaelewa jambo gani likae kwenye fahamu zetu kwa muda mrefu na lipi likiingia tu tujitahidi kuliondoa mara moja lisije likaharibu fahamu zetu. Ninaelewa kuwa utakuwa unawaza kuwa ni vigumu kuyatoa baadhi ya mambo akilini mwako, lakini kuna mbinu za kuweza kufanya hivyo. Kwa kuwa mbinu hizo siyo sehemu ya makala hii basi zitajadiliwa katika makala zijazo. Lakini la muhimu hapa ni kuwa kwa kuwa kila kitu tunachoweka katika fahamu zetu hujenga tabia, imani na hata miujiza basi tukiweza mambo mema kama mafanikio na tukafuata mbinu zote na sayansi ya mafanikio basi mafanikio yatakuja kama muujiza kama vile mtoto anavyoweza kuzungumza lugha fulani lakini bila kujifunza kwa kutoa jasho jingi. Na mafanikio yanayofata taratibu na sheria hizi zilizosahaurika kwa muda mrefu hazihitaji mtu atoe maji na damu ndiyo afanikiwe. Akifuata taratibu hizi na nyingine nyingi zilizoko katika sayansi ya mafanikio basi hufanikiwa kimiujiza.

Uzuri wa sayansi imebaki katika baadhi ya imani za kidini. Umewahi kuona watu wanaposali kwa kutumia vifaa furani ili kuweza kukariri maneno fulani fulani? Au umewahi kwenda kwa mganga wa kienyeji akakuambia uzngumze maneno fulani ubayotaka yatokee mara mia moja? Angalia hata makanisani ziku hizi sara zinavyofanywa, ni kurudia maneno kwa muda mrefu ili kuujenga ufahamu ukubali yale ambayo Mungu anataka kukufanyie. Au kamuulize Joshua wakati wa Musa, jinsi sayansi hii ilivyofanya kazi. Kwamba maneno haya yasitoke kinywani mwako, uyaseme usiku na mchana, utende kulingana na hayo (Effecient Actions).

Ni vizuri tukaanza basi kuzilisha fahamu zetu yale tunayopenda yatokee katika maisha yetu. Juzi wakati wa mfungo wa Ramadhan, shehe aliwakumbusha habari ya kufunga na kunuia kile unachokitaka. Kunuia ndiyo mwanzo wa miuujiza. Ugumu unakuwa jinsi ya kuweza kunuia jambo lako unalolitaka. Sayansi hii haifundishwa madarasani wa vyuo vikuu. Nchi kama marekani na ulaya masomo haya hupatika kw aurahisi labda ndiyo yamewasaidi sayansi hii na mafanikio yao unaweza kuyaona. a kufika pale walipo. Makala ijayo tutatafakari pamoja jinsi ya kuchagua kitu ambacho kinapaswa kiingizwe kwenye ufahamu wako nakujifunza sayansi ya mafanikio ili kilete mafanikio unayokusudia.

Elizabethrose Memorial Institue amedhamiria kutoa mafunzo ya Mafanikio ya Maisha ili kuweza kuwasaidia wengi wanaoteseka katika dimbi la umasiki huku wakisubiria serikali iwafanyie kila jambo. Tafadhali makala hii ikikuguza wasaliana nasi tukuoneshe jinsi ya kutengeneza muujiza wako BURE. Mafunzo haya hayalipiwi maana tunaamini kuwa ukitaka kufanikiwa basi saidia wengi.