Ijumaa, 16 Septemba 2011

Je Unaweza Kutengeneza Muujiza Wako?

Je unaweza kutengeneza muujiza wako? Si umeshudia matangazo mengi ya miujiza kuanzia makanisani, miskitini hadi kwa waganga wa kienyeji wote wakitangaza miujiza? Je unafahamu miujiza unavyofanyika? Unafahamu mungu wako anavyokutengenezea muujiza wako?  Miujiza hili inaweza kutokea katika imani yoyote.

Tumezungumza kuwa ufahamu(mind) ikilishwa vizuri inaweza ikafanya jambo lolote. Chakula cha ufahamu, kama nilivyosema kwenye makala iliyotangulia, ni mambo chanya (positive) ambayo tunayaingiza kwenye fahamu zetu. Nilikwenda mbali zaidi nikasema hata miujiza mingi huanzia kwenye ufahamu. Mfano mzuri wa muujiza ulioanzia kwenye ufahamu ni ule wa Daudi, mtoto mdogo kumpiga Goliath Jemedari wa vita. Pia nilizungumza jinsi ambavyo watu wametumia vibaya fahamu zao na kusababisha miujiza mibaya katika maisha yao. Kwa mfano kunuia ugonjwa kwa muda mrefu lazima utakujia, kunuia kifo, lazima kitakufika n.k. Leo napenda tuangalie jinsi fahamu zetu zinavyosababisha miujiza kama tukiweza kuzilisha mambo mema. Kama nilivyosema ufahamu (mind) zina sehemu mbili yaani conscious na subconscious. Hizi zina tabia mbili tofauti. Tuziangalie tabia za sehemu hizi mbili tofauti za ufahamu.

1. Conscious Mind
Sehemu hii ya ufahamu hutengenezwa na viungo vile vitano vya fahamu  kama tulivyosoma zamani kwenye sayansi au biologia. Hivi ni macho kwa kuona, pua kwa kunusa, mwili kwa kuhisi, sikio kwa kusikia na ulimi kwa kuonja. Taarifa zote zinazoingia kwenye ufahamu hupitia kwenye ufahamu wa conscious. Tafiti zinaonesha kuwa taarifa zinazoingia kupitia ufahamu huu huchukua sekunde moja hadi mbili kutulia kwenye akili/ufahamu wetu. Ndiyo maana unakuta kwa siku mtu anakuwa na fikra nyingi nyingi zilizoingizwa kwenye ufahamu kupitia viungo hivyo. Kwa kuwa fikra zinazoingia kwenya akili/fahamu zetu kwa mtindo huu hukaa hapo muda mfupi, basi hizi hazitusaidie chochote. Haziwezi kujenga imani wala haziwezi kujenga tabia ya mtu. Hivyo ni vizuri tusiruhusu au kudhubiti vitu ambavyo vinatakiwa kuingia kwenye akili zetu.

2. Subconscious Mind.
Hii ni sehemu ya pili ya jinsi fahamu zetu zinavyofanya kazi. Sehemu hii hupokea taarifa zote kutoka kwenye conscious mind ambazo zimekaa pale kwa muda mrefu. Sehemu hii hutoa matokea yanayolingana na taarifa ilizozipokea, pia ndiyo sehemu hutengeneza tabia zote za binadamu kama taarifa hizo zikikaa hapa muda mrefu. Kwa mfano, kupitia vile viungo vya fahamu, kama taarifa moja ikikaa pale muda mrefu(kufikiria taarifa kwa muda mrefu) basi taarifa hiyo iwe nzuri au mbaya itakutokea tu. Sehemu hii unaweza kujua inavyofanya kazi kama vile mtoto anavyojifunza lugha. Hujifunza kwa kusikia muda mrefu na kurudia rudia. Kama nilivyosema sehemu hii haichagua baya wa zuri, unachoweka ndicho hukuletea. Kama umeweka kwamba kwenu mmelaani na hamuwezi kufanikiwa, au kuwa viongozi au hata kufaulu mitihani basi fahamu hizo zinakusaidia kuamini hivyo. Ufahamu huu pia ukiulisha kufanikiwa na kukiri kuwa jambo fulani uliweza kwa kurudia rudia basi jambo hilo litatoke hivyo.

Kwa hiyo basi ni vizuri tukaelewa jambo gani likae kwenye fahamu zetu kwa muda mrefu na lipi likiingia tu tujitahidi kuliondoa mara moja lisije likaharibu fahamu zetu. Ninaelewa kuwa utakuwa unawaza kuwa ni vigumu kuyatoa baadhi ya mambo akilini mwako, lakini kuna mbinu za kuweza kufanya hivyo. Kwa kuwa mbinu hizo siyo sehemu ya makala hii basi zitajadiliwa katika makala zijazo. Lakini la muhimu hapa ni kuwa kwa kuwa kila kitu tunachoweka katika fahamu zetu hujenga tabia, imani na hata miujiza basi tukiweza mambo mema kama mafanikio na tukafuata mbinu zote na sayansi ya mafanikio basi mafanikio yatakuja kama muujiza kama vile mtoto anavyoweza kuzungumza lugha fulani lakini bila kujifunza kwa kutoa jasho jingi. Na mafanikio yanayofata taratibu na sheria hizi zilizosahaurika kwa muda mrefu hazihitaji mtu atoe maji na damu ndiyo afanikiwe. Akifuata taratibu hizi na nyingine nyingi zilizoko katika sayansi ya mafanikio basi hufanikiwa kimiujiza.

Uzuri wa sayansi imebaki katika baadhi ya imani za kidini. Umewahi kuona watu wanaposali kwa kutumia vifaa furani ili kuweza kukariri maneno fulani fulani? Au umewahi kwenda kwa mganga wa kienyeji akakuambia uzngumze maneno fulani ubayotaka yatokee mara mia moja? Angalia hata makanisani ziku hizi sara zinavyofanywa, ni kurudia maneno kwa muda mrefu ili kuujenga ufahamu ukubali yale ambayo Mungu anataka kukufanyie. Au kamuulize Joshua wakati wa Musa, jinsi sayansi hii ilivyofanya kazi. Kwamba maneno haya yasitoke kinywani mwako, uyaseme usiku na mchana, utende kulingana na hayo (Effecient Actions).

Ni vizuri tukaanza basi kuzilisha fahamu zetu yale tunayopenda yatokee katika maisha yetu. Juzi wakati wa mfungo wa Ramadhan, shehe aliwakumbusha habari ya kufunga na kunuia kile unachokitaka. Kunuia ndiyo mwanzo wa miuujiza. Ugumu unakuwa jinsi ya kuweza kunuia jambo lako unalolitaka. Sayansi hii haifundishwa madarasani wa vyuo vikuu. Nchi kama marekani na ulaya masomo haya hupatika kw aurahisi labda ndiyo yamewasaidi sayansi hii na mafanikio yao unaweza kuyaona. a kufika pale walipo. Makala ijayo tutatafakari pamoja jinsi ya kuchagua kitu ambacho kinapaswa kiingizwe kwenye ufahamu wako nakujifunza sayansi ya mafanikio ili kilete mafanikio unayokusudia.

Elizabethrose Memorial Institue amedhamiria kutoa mafunzo ya Mafanikio ya Maisha ili kuweza kuwasaidia wengi wanaoteseka katika dimbi la umasiki huku wakisubiria serikali iwafanyie kila jambo. Tafadhali makala hii ikikuguza wasaliana nasi tukuoneshe jinsi ya kutengeneza muujiza wako BURE. Mafunzo haya hayalipiwi maana tunaamini kuwa ukitaka kufanikiwa basi saidia wengi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni