Jumatatu, 19 Septemba 2011

Je Unajua Kama Kuna Mbinu za Kutajirika?


Kuna NGUVU ambayo kila kitu kiliumbwa kutoka  kwake, ambacho kwa asili yake inaruhusu, inapitisha na kuujaza uwazi ulioko katika ulimwengu. 

Wazo linalokuwa katika NGUVU hiyo huzalisha kitu ambacho kimefikiriwa katika wazo hilo. 

Mtu anaweza kutengeneza wazo lake na kwa kuliweka katika NGUVU hiyo isiyokuwa na umbo anaweza kusababisha kitu anachokifikiri kutengenezwa. 

Ili kuweza kufanya haya, mtu lazima atoke katika hali ya ushindani na aingie katika hali ya ufahamu wa ubunifu. Bila hivyo hawezi kwenda sambamba na NGUVU hiyo ambayo siku zote ni bunifu na wala haina roho ya ushindani.  

Mtu anaweza kwenda sawa na NGUVU hii kwa kuwa na shukurani ya kweli kwa baraka ambazo amewahi kupata. Shukurani huunganisha ufahamu wa mtu na akili ya NGUVU ili wazo la mtu liweze kupokelewa na NGUVU hiyo.

Mtu anaweza kubaki katika hali ya ubunifu kama tu akijiunganisha na akili ya NGUVU kupitia hisia za ndani na za siku zote za shukurani. 

Mtu anaweza kutengeneza picha ya vitu anavyotaka kuvipata, kuvifanya au unavyotaka kuwa na ni lazima kushikiria picha ya vitu hicho katika mawazo yake na kuwa na shukurani za ndani kwa NGUVU kwamba amepata hitaji lake. Mtu anayetaka kuwa kuwa tajiri lazima atumie muda wake kufikiria ndoto yake na shukurani kuwa amepokea kile anachokitaka.


Umewahi kuona watu wa elimu sawa, mazingira sawa, biashara sawa na kila kitu kiko sawa, lakini mmoja anakuwa tajiri mwingine fukara wa kutupwa? Au umewahi kuona wale waliokuwa na akili sana darasani wanakuwa masikini huku mbumbumbu wa kutupwa anakuwa tajiri? 

Kuna sayansi na njia sahihi za kuwa tajiri. Hizi zikifuatwa kwa usahihi lazima mtu atakuwa tajiri. Haihitaji uwe New York au London au Paris au kokote walikoendelea ndiyo uwe tajiri. Ndiyo maana hata huko kuna masikini wakubwa wakati Tanzania pia kuna mabilionea na masikini. Hata jagwa la sahara pamoja na ukame kuna matajiri pia. Hivyo kuna mbinu za kuwa tajiri.

Hivyo ni jukumu la kila mtu kujifunza mbinu hizi na sayansi ya kupata utajiri. Elizabethrose Memorial Institute imedhamiria kufundisha wajisiriamali njia sahihi za kupata mafanikio BURE. Maana tunaamini ili kufanikiwa lazima usaidie wengi. Wasiliana wasi tukusaidie.

Ijumaa, 16 Septemba 2011

Je Unaweza Kutengeneza Muujiza Wako?

Je unaweza kutengeneza muujiza wako? Si umeshudia matangazo mengi ya miujiza kuanzia makanisani, miskitini hadi kwa waganga wa kienyeji wote wakitangaza miujiza? Je unafahamu miujiza unavyofanyika? Unafahamu mungu wako anavyokutengenezea muujiza wako?  Miujiza hili inaweza kutokea katika imani yoyote.

Tumezungumza kuwa ufahamu(mind) ikilishwa vizuri inaweza ikafanya jambo lolote. Chakula cha ufahamu, kama nilivyosema kwenye makala iliyotangulia, ni mambo chanya (positive) ambayo tunayaingiza kwenye fahamu zetu. Nilikwenda mbali zaidi nikasema hata miujiza mingi huanzia kwenye ufahamu. Mfano mzuri wa muujiza ulioanzia kwenye ufahamu ni ule wa Daudi, mtoto mdogo kumpiga Goliath Jemedari wa vita. Pia nilizungumza jinsi ambavyo watu wametumia vibaya fahamu zao na kusababisha miujiza mibaya katika maisha yao. Kwa mfano kunuia ugonjwa kwa muda mrefu lazima utakujia, kunuia kifo, lazima kitakufika n.k. Leo napenda tuangalie jinsi fahamu zetu zinavyosababisha miujiza kama tukiweza kuzilisha mambo mema. Kama nilivyosema ufahamu (mind) zina sehemu mbili yaani conscious na subconscious. Hizi zina tabia mbili tofauti. Tuziangalie tabia za sehemu hizi mbili tofauti za ufahamu.

1. Conscious Mind
Sehemu hii ya ufahamu hutengenezwa na viungo vile vitano vya fahamu  kama tulivyosoma zamani kwenye sayansi au biologia. Hivi ni macho kwa kuona, pua kwa kunusa, mwili kwa kuhisi, sikio kwa kusikia na ulimi kwa kuonja. Taarifa zote zinazoingia kwenye ufahamu hupitia kwenye ufahamu wa conscious. Tafiti zinaonesha kuwa taarifa zinazoingia kupitia ufahamu huu huchukua sekunde moja hadi mbili kutulia kwenye akili/ufahamu wetu. Ndiyo maana unakuta kwa siku mtu anakuwa na fikra nyingi nyingi zilizoingizwa kwenye ufahamu kupitia viungo hivyo. Kwa kuwa fikra zinazoingia kwenya akili/fahamu zetu kwa mtindo huu hukaa hapo muda mfupi, basi hizi hazitusaidie chochote. Haziwezi kujenga imani wala haziwezi kujenga tabia ya mtu. Hivyo ni vizuri tusiruhusu au kudhubiti vitu ambavyo vinatakiwa kuingia kwenye akili zetu.

2. Subconscious Mind.
Hii ni sehemu ya pili ya jinsi fahamu zetu zinavyofanya kazi. Sehemu hii hupokea taarifa zote kutoka kwenye conscious mind ambazo zimekaa pale kwa muda mrefu. Sehemu hii hutoa matokea yanayolingana na taarifa ilizozipokea, pia ndiyo sehemu hutengeneza tabia zote za binadamu kama taarifa hizo zikikaa hapa muda mrefu. Kwa mfano, kupitia vile viungo vya fahamu, kama taarifa moja ikikaa pale muda mrefu(kufikiria taarifa kwa muda mrefu) basi taarifa hiyo iwe nzuri au mbaya itakutokea tu. Sehemu hii unaweza kujua inavyofanya kazi kama vile mtoto anavyojifunza lugha. Hujifunza kwa kusikia muda mrefu na kurudia rudia. Kama nilivyosema sehemu hii haichagua baya wa zuri, unachoweka ndicho hukuletea. Kama umeweka kwamba kwenu mmelaani na hamuwezi kufanikiwa, au kuwa viongozi au hata kufaulu mitihani basi fahamu hizo zinakusaidia kuamini hivyo. Ufahamu huu pia ukiulisha kufanikiwa na kukiri kuwa jambo fulani uliweza kwa kurudia rudia basi jambo hilo litatoke hivyo.

Kwa hiyo basi ni vizuri tukaelewa jambo gani likae kwenye fahamu zetu kwa muda mrefu na lipi likiingia tu tujitahidi kuliondoa mara moja lisije likaharibu fahamu zetu. Ninaelewa kuwa utakuwa unawaza kuwa ni vigumu kuyatoa baadhi ya mambo akilini mwako, lakini kuna mbinu za kuweza kufanya hivyo. Kwa kuwa mbinu hizo siyo sehemu ya makala hii basi zitajadiliwa katika makala zijazo. Lakini la muhimu hapa ni kuwa kwa kuwa kila kitu tunachoweka katika fahamu zetu hujenga tabia, imani na hata miujiza basi tukiweza mambo mema kama mafanikio na tukafuata mbinu zote na sayansi ya mafanikio basi mafanikio yatakuja kama muujiza kama vile mtoto anavyoweza kuzungumza lugha fulani lakini bila kujifunza kwa kutoa jasho jingi. Na mafanikio yanayofata taratibu na sheria hizi zilizosahaurika kwa muda mrefu hazihitaji mtu atoe maji na damu ndiyo afanikiwe. Akifuata taratibu hizi na nyingine nyingi zilizoko katika sayansi ya mafanikio basi hufanikiwa kimiujiza.

Uzuri wa sayansi imebaki katika baadhi ya imani za kidini. Umewahi kuona watu wanaposali kwa kutumia vifaa furani ili kuweza kukariri maneno fulani fulani? Au umewahi kwenda kwa mganga wa kienyeji akakuambia uzngumze maneno fulani ubayotaka yatokee mara mia moja? Angalia hata makanisani ziku hizi sara zinavyofanywa, ni kurudia maneno kwa muda mrefu ili kuujenga ufahamu ukubali yale ambayo Mungu anataka kukufanyie. Au kamuulize Joshua wakati wa Musa, jinsi sayansi hii ilivyofanya kazi. Kwamba maneno haya yasitoke kinywani mwako, uyaseme usiku na mchana, utende kulingana na hayo (Effecient Actions).

Ni vizuri tukaanza basi kuzilisha fahamu zetu yale tunayopenda yatokee katika maisha yetu. Juzi wakati wa mfungo wa Ramadhan, shehe aliwakumbusha habari ya kufunga na kunuia kile unachokitaka. Kunuia ndiyo mwanzo wa miuujiza. Ugumu unakuwa jinsi ya kuweza kunuia jambo lako unalolitaka. Sayansi hii haifundishwa madarasani wa vyuo vikuu. Nchi kama marekani na ulaya masomo haya hupatika kw aurahisi labda ndiyo yamewasaidi sayansi hii na mafanikio yao unaweza kuyaona. a kufika pale walipo. Makala ijayo tutatafakari pamoja jinsi ya kuchagua kitu ambacho kinapaswa kiingizwe kwenye ufahamu wako nakujifunza sayansi ya mafanikio ili kilete mafanikio unayokusudia.

Elizabethrose Memorial Institue amedhamiria kutoa mafunzo ya Mafanikio ya Maisha ili kuweza kuwasaidia wengi wanaoteseka katika dimbi la umasiki huku wakisubiria serikali iwafanyie kila jambo. Tafadhali makala hii ikikuguza wasaliana nasi tukuoneshe jinsi ya kutengeneza muujiza wako BURE. Mafunzo haya hayalipiwi maana tunaamini kuwa ukitaka kufanikiwa basi saidia wengi.

Jumanne, 13 Septemba 2011

VYOTE VILIANZA KAMA WAZO.

Je, umewahi kujiuliza ni kwa jinsi gani vitu vyote humu ulimwenguni viliumbwa? Je, wanadamu waliumbwa kutokea nini au wapi? Haya ni maswali ya muhimu ambayo wewe kama mwanadamu unapaswa kujiuliza na mwisho wa siku kupata majibu sahihi. Lengo langu hapa sio kujadiliana na wewe kuhusu vitu vilivyotumika kuutengeneza ulimwengu au kuwaumba wanadamu, la hasha, kwani kwa kufanya hivyo hatutaweza kuumaliza mjadala huo sababu nitakuuliza ni wapi hivyo vitu vilivyotumika kutengenezea (yaani malighafi) vilipotokea. Nia yangu ni kutaka kukushirikisha juu ya nilichogundua kuhusiana na ukweli huu kuwa “kila kitu kilianza kama wazo”.

Tukiuangalia uumbaji kutoka katika mitazamo ya baadhi ya dini zetu tunagundua kuwa wote na vyote ulimwenguni humu viliumbwa na Mungu. Bila shaka utakubaliana na mimi kuwa kabla Mungu hajaamua kuiumba dunia na wanadamu aliwaza kwanza. Aliuwaza uwepo wa nchi kavu ndipo akaziumba, aliuwaza uwepo wa makusanyiko yote ya maji yaani bahari, maziwa, mito na yote yafananayo na hayo ndipo alipoviumba. Hata wanyama na wanadamu vivyo hivyo, bila kusahau vitu vyote ambavyo wewe unaviita ni vya asili vilitokana na mawazo kwanza kabla ya kuumbwa kwake.

Tukiachana na uumbaji wa Mungu, hebu na tuuangalie uumbaji wa wanandamu. Vitu vyote visivyo vya asili vimetengenezwa na wanadamu wenyewe, kwa mfano nyumba kwa mitindo yake yote kuanzia maghorofa hadi zile za jadi. Magari, mavazi hata vyombo vya nyumbani ni baadhi tu ya vitu vilivyotengenezwa na wanandamu. Hebu ichunguze hiyo computer unayoitumia, hicho kiti ulichokikalia na hayo mavazi uliyoyavaa, umegundua nini? Hayo yote ni mawazo ya watu, kabla hawajavitengeneza  waliwaza kwanza. Kuwaza kitu ni kukiona hicho kitu kwa wakati ujao. Aliyegundua viatu alianza kuwaza  na ndipo aliwaona watu wamevaa viatu hata kabla viatu hivyo havijatengenezwa. Kila kitu unachokiona na kukitumia ni wazo la mtu, kilianza kama wazo, kikatendewa kazi ndipo kikadhihirika kuwa mali au bidhaa bora. Wazo lolote unalolipata litendee kazi pasipo kuyakaribisha mawazo hasi. Jaribu kuwaza hivi kama Mungu angewaza hasi kabla ya kutuumba, mimi na wewe tungeumbwa? Pamoja na ukweli kuwa mimi na wewe tunamkosea kila siku aliyetuumba, hiyo haijawa sababu ya yeye kujuta kutuumba na kuutowesha kabisa uumbaji wake badala yake wanadamu wazidi ongezeka. Je, kuna haja gani ya mimi na wewe kuyatowesha mawazo mazuri ya maendeleo eti kisa tu tunayaruhusu mawazo hasi akilini mwetu?

Ninahitimisha  kwa kusema kuwa kila mtu anaweza na anayo haki ya kuyafurahia matunda yatokanayo na mawazo na mitazamo yake. Hili litawezekana tu iwapo tutawaza kwa usahihi na kwa mitazamo chanya ya kijasiriamali daima.

SHAUKU YAKO NDIO MTAJI WAKO.

Shauku ni kiu au hamu ya kutaka kukijua au kukipata kitu Fulani. Shauku inaweza ikaleta manufaa ikitumiwa vizuri. Leo ninapenda kuongelea shauku ambayo watu wengi wanayo ila mimi ninajikita zaidi katika ile shauku iliyojengwa katika misingi chanya zaidi kwa mfano, shauku ya kutaka kujua wewe ni nani na kusudi lako hapa duniani ni lipi?

Kila mwanadamu aliyeko chini ya jua analo kusudi lake aliloitiwa kulifanya hapa duniani, hili ni jambo la kulichunguza kwa umakini na kulipatia ufumbuzi, ninasema ufumbuzi kwa sababu kitendo cha wewe kutojifahamu au kutolitambua kusudi lako hapa duniani ni tatizo kubwa sana. Ukweli ni kwamba kila mtu analo eneo lake analotosheleza vizuri yaani analoweza kulifanyia kazi vizuri zaidi katika Nyanja mbalimbali.
Kabla ya kulijua eneo unalotosheleza ni vizuri uwe umepitia au umejiruhusu kuwepo katika mazingira yafananayo na eneo hilo kwa mfano, ili kujua kama wewe ni mzuri katika mambo ya saluni ni vizuri uwe umekaa maeneo ambayo shughuli zinazofanyika saluni huwa zinafanyika na hapo hata kama zinafanywa katika mazingira yasiyo rasmi. Ni vigumu kumkuta mtu aliyekulia katika jamii ambayo wanawake na wanaume wananyoa vipara vya wembe kila wakati na hawaamini katika kusuka au kutengeneza nywele kwa mtindo wowote ule akawa mtaalamu katika mambo ya urembo wa nywele, kama kuna watu kama hao, basi ni wachache sana.

Uzoefu unaonyesha kuwa watu waliozaliwa au kukulia maeneo yanayozungukwa au karibiana na vitu kama bahari, mito na maziwa ni wazuri sana katika kuogelea au shughuli zinazohusiana na uvuvi kuliko wale waliozaliwa sehemu kame.

Eneo unalotesheleza litaeleweka vizuri nikiliita “kipaji”. Kipaji chako ndio maisha yako, mtaji wako na ndio eneo lako litakalokutoa kimaisha, nikisema litakalo “kutoa” namaanisha litakalokusababishia upande au ufanye vizuri kimaisha. Kipaji chako kitakuwa na nguvu zaidi kikigunduliwa na wewe mwenyewe, na ili ukijue ni lazima uwe na “shauku” ya kukigundua hasa kwa kuanza kujichunguza ni kusudi gani  unahisi unalo hapa duniani. Shauku yako ikiwa kubwa ndipo uwezekano wa wewe kugundua kipaji zaidi ya kimoja ndani yako unapotokea. Ni kitu gani hasa unapendelea kukifanya na unaweza kukifanya na unasikia amani na furaha kukifanya? Huenda hicho ndicho kipaji chako na kinahitaji kukuzwa. Kipaji ni zawadi aliyopewa mtu tangu kuumbwa kwake, sio kitu cha kuiga kutoka kwa mtu mwingine. Kipaji pia sio lazima kitokane na mazingira aliyokulia mtu kwani vitu vingine vinavyoitwa vipaji sio vipaji, ni ujuzi tu mtu aliojifunza au anaouiga na hii huwa haileti matokeo mazuri. Nahitimisha kwa kusema “kuwa na shauku ya kukijua kipaji chako”.