Alhamisi, 25 Agosti 2011

Walioko Nyuma ya EMI

Enock Mayage :CPA (T), Msc in Auditing and Consultancy (UK).
Mayage amejikita sana katika kuwafundisha wajasiriamali wanaoanza na wale ambao tayari wameanza. Ni mtalaam wa fani ya uhasibu na ukaguzi wa mahesabu na ushauri, utalaam aliousomea nchini Uingereza. Pia amejikita katika kuhamasisha na kutia moyo juu ya maisha na ubunifu wa biashara. Amekuwa mzungumzaji (public speaker) katika makongamano ya ndani na nje ya nchi juu ya biashara na mafanikio. Mayage anaamini mtu yeyote anaweza kupata kile anachokitaka. Mafundisho haya yanasimama kwenye kanuni iliyotumiwa na akila Henry Ford, Edson, Oprah, Anderson, John Assaraf, Bob Proctor, Jim Rohn, Tony Robins na wengine kujipatia mafanikio makubwa. Falsafa zinazotumika katika mafunzo haya ni za watu mashuhuri duniani kama akina Nelson Mandela, M.Ghandi, JK Nyerere, F.Kennedy n.k ambao waliamini kuwa ukitaka kufanikiwa saidia kwanza wengi.

Herieth K. Mushi
Ni Meneja na Masoko wa Tasisi. Amefanya kazi na Tasisi kwa muda mrefu kwa kuwasaidia wateja wengi katia biashara zao. Herieth pia ameakuwa mzungumzaji wa maswala ya ujasiriamali ambapo amewasaidia wengi kubadilisha mitazamo yao juu ya maswala ya ujasiriamali. Pia amewahi kufanya kazi na mashirika mbalimbali za kitaifa na kimataifa yanayojihusisha na ujasiriamali kama vile Shirika la Umoja wa Mataifa na Maendeleo ya Viwanda na Biashara (UNIDO) katika mradi wa Africa Investor Survey.

Regina E. Pandisha
Ni Msaidizi wa Mtendaji Mkuu. Amekuwa na Tasisi kwa muda
mrefu. Ni mzoefu na mzungumzaji wa maswala ya ujasiriamali. Regina ameandaa mikutano mingi ya wajasiriamali.

Unajua Kama Una Haki ya Kuwa Tajiri?

Mambo yote yamesemwa juu ya kutukuza umasikini, hoja inabaki pale pale kuwa huwezi kuishi maisha timilifu na yenye mafanikio bila kuwa tajiri. Hakuna anayeweza kufikia hatua ya juu kabisa katika vipaji vyake au kukua kiroho isipokuwa ana fedha nyingi, kwa kuwa kukuza roho na kipaji lazima uwe na fedha nyingi, na huwezi kuvipata vitu hivyo mpaka uwe na fedha za kuvinunua. Mtu huendeleza akili, roho na mwili kwa kutumia vitu, na jamii imejipanga kutuwezesha kuvipata vitu hivyo.

Jumatatu, 22 Agosti 2011

Nini Utegemee Kupata Unapokuja Kujifunza Nasi.

Elizabethrose Memorial Institute imedhamiria kuwasaidia watanzania wengi katika kuanzisha na kusimamia biashara hapa nchini. Katika research ambayo tulifanya hivi karibuni tuligundua kuwa biashara nyingi ndogo ndogo hapa nchini huanzishwa kwa kuiga na siyo hutokana na vipaji ambavyo mhusika anacho. Elizabethrose Memorial Institute inaamini kuwa kila binadamu ana vipaji vyake ambavyo akivitambua na kuvisisimua anaweza kuanzisha biashara ambayo inaweza kuwa endelevu na ya aina yake.

Tulipojiuliza kwa nini wajasiriamali wengi hawawezi kubuni biashara tofauti jibu lilikuwa kwamba mfumo wa maisha ambao tulikuwa nao hapa nchini inawezekana ndiyo umesababisha ubunifu wetu ukawa mdogo. Kwa mfano tuliamini katika kuwa na mitaji ya pamoja katika ujamaa, hivyo kuwa na duka la kaya, kusoma shule za aina moja, hospitali za aina moja na kadhalika. Haya mambo yalikuwa mazuri sana kama yangeweza kufanikiwa kama yalivyokuwa yamekusudiwa katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Mantiki kubwa katika ujamaa ilikuwa kumiliki mitaji kwa pamoja, hivyo mtu mmoja mmoja hakuweza kupata nafasi ya kumiliki mitaji. Hata wale waliokuwa wamiliki wa mitaji walionekana kama wanyonyaji katika jamii. Tofauti na ubepari ambao uliamini katika mtu mmoja mmoja kumiliki mtaji wake.

Kuna matatizo ambayo yalitokea katika kusimamia mitaji yetu ambayo mingi iliwekwa katika mashirika ya umma ambapo baadaye wajanja wachache tuliowaamini wasimamie mitaji kwa niaba yetu waliamua kuimaliza mitaji yetu na ndiyo maana mashirika ya umma yamekwisha kabisha. Tofauti na hilo, pia watu wengi hawakuweza kujishughulisha na ubunifu wa biashara kwa kuwa nafasi hiyo hakuwepo. Matokeo ya akili zetu kutojishughulisha katika ubunifu wa biashara yako wazi tu. Kwa uchache nitaje machache tu.
1. Kwa nini leo ukitafuta biashara za kufundisha kiswahili kwa wageni utakuta Kenya na Uganda wanayo mengi wakati kiswahili ni lugha yetu watanzania?
2. Leo ukitafuta mashirika yanayopandisha watalii wengi mlima Kilimanjaro utakuwa wakenya wanaongoza wakati mlima Kilimanjaro ni wa watanzania?
3. Uliwahi kuchunguza kwa nini wakenya waliweka picha video nyingi kwenye YOUTUBE kumutangaza  Babu wa Loliondo alipovuma?
Huu ni baadhi ya ubunifu ambao wenzetu wanaotumia kuanzisha biashara hivyo kufanya kuleta ushindani wa mkubwa wa biashara katika Afrika Mashariki.

Inatupasa tukubali tulipokwama na kuanza kufanya marekebisho makubwa ili tuweze kushindana katika soko huria. Mara zote nawambia wanafunzi wangu kuwa masomo ya ujasiriamali hapa kwetu yameanza miaka michache iliyopita. Hata yale tunayojifunza katika ujasiriamali siyo aliyopaswa kufundisha huyu anayeanza biashara. Masomo mengi ya ujasiriamali ambayo hufundishwa hapa nchini ni kutunza vitabu ya kihasibu, kuandaa michanganuo ya biashara na kutayarisha taarifa za kodi. Kwa mjasiriamali anayeanza haya si sawa kujifunza. Ni vizuri taasisi zote zinazotoa mafunzo ya ujasiriamali zikaanza na kuwaelimisha watu juu umuhimu wa kujua kipaji chako na kukisisimua ili biashara yako itoke huko. Ni vizuri watanzania hawa ambapo madhara ya kumiliki mitaji kwa pamoja bado wanayo wakafundishwa kuwa sasa tumetoka huko sasa tuko kwenye soko huria.(Mind Set).

Sisi katika Elizabethrose Memorial institute tunaamini kuwa jambo la kwanza kabisa kwa mjasiriamali anayeanza nikumweka sawa kiakili ili aachane na yale tayari ambayo alikuwa anaamiki katika kufanya biashara. Tunamjenga kisaikolojia ili aweze kujiamini na kuona kuwa anaweza. Hii inamsaidia kuchangua na kupata malengo yake ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu. Masomo yetu yamegawanika katika sehemu tatu:

1. Business Coaching.
Hii ni kama kocha wa mpira anavyomfundisha mchezaji kucheza mpira. Hufanyika kwa vitengo hasa tukianza na kutambua kipaji cha mhusika na kukitumia katika kuchagua biashara anayoweza kuifanya. Mara nyingi watu huuliza kuwa tunawezaji kupambua vipaji vya watu? Hili tunalifanya pamoja na mhusika kwa kurudi nyuma tangia alipokuwa darasa la kwanza hadi la saba alipenda kufanya nini, na alisifiwa kwa kufanya nini. Kwa kutafakari kwa pamoja mwisho tunajua mtu huyu Mungu alimleta duniani kwa sababu gani.

2. Busness Mentoring.
Hapa tunashughulika na mtu ambaye tayari ameanza biashara lakini anashindwa kukua. Tunachofanya tunamtafutia mtu aliyefanikiwa katika biashara hiyo na kumuunganisha naye ili aweze kuiga wenzake wanafanyaji katika hiyo biashara.

3. Business Consultancy
Hapa ndipo pale tunaangalia biashara kawa ujumla wake; kuanzia kwenye mkakati wa biashara (strategy), malengo na utekelezaji wake na kutoa ushari juu ya maswala ya uhasibu, ukaguzi wa hesabu na maswala ya kodi. Hii ni hatua ya juu ambapo mjasiriamali anakuwa ameshakuwa hivyo kuhitaji huduma hizi.

Naomba hili niliweke sawa, biashara inaweza kuanzishwa katika kipaji chochote. Tunaweza kukusaidia katika eneo lolote kuanzia biashara, michezo, kuigiza, kuimba. Kuwa wale wanaotaka kuonekana hata kwenye luninga tunaweza kufanya kazi na wewe mpaka ukawa celebrity. Tujaribu onone huduma zetu. Na la mwisho ambalo ni tofauti na wengine hatukulipishi ada yoyote mpaka pale utakapoanza kufanikiwa katika biashara yako.Tutafute Tukue Pamoja.

Tunapatikana Ubungo Riverside karibu na kanisa la Father Kwera ukifika pale wewe tuulizie tu.