Elizabethrose Memorial Institute imedhamiria kuwasaidia watanzania wengi katika kuanzisha na kusimamia biashara hapa nchini. Katika research ambayo tulifanya hivi karibuni tuligundua kuwa biashara nyingi ndogo ndogo hapa nchini huanzishwa kwa kuiga na siyo hutokana na vipaji ambavyo mhusika anacho. Elizabethrose Memorial Institute inaamini kuwa kila binadamu ana vipaji vyake ambavyo akivitambua na kuvisisimua anaweza kuanzisha biashara ambayo inaweza kuwa endelevu na ya aina yake.
Tulipojiuliza kwa nini wajasiriamali wengi hawawezi kubuni biashara tofauti jibu lilikuwa kwamba mfumo wa maisha ambao tulikuwa nao hapa nchini inawezekana ndiyo umesababisha ubunifu wetu ukawa mdogo. Kwa mfano tuliamini katika kuwa na mitaji ya pamoja katika ujamaa, hivyo kuwa na duka la kaya, kusoma shule za aina moja, hospitali za aina moja na kadhalika. Haya mambo yalikuwa mazuri sana kama yangeweza kufanikiwa kama yalivyokuwa yamekusudiwa katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Mantiki kubwa katika ujamaa ilikuwa kumiliki mitaji kwa pamoja, hivyo mtu mmoja mmoja hakuweza kupata nafasi ya kumiliki mitaji. Hata wale waliokuwa wamiliki wa mitaji walionekana kama wanyonyaji katika jamii. Tofauti na ubepari ambao uliamini katika mtu mmoja mmoja kumiliki mtaji wake.
Kuna matatizo ambayo yalitokea katika kusimamia mitaji yetu ambayo mingi iliwekwa katika mashirika ya umma ambapo baadaye wajanja wachache tuliowaamini wasimamie mitaji kwa niaba yetu waliamua kuimaliza mitaji yetu na ndiyo maana mashirika ya umma yamekwisha kabisha. Tofauti na hilo, pia watu wengi hawakuweza kujishughulisha na ubunifu wa biashara kwa kuwa nafasi hiyo hakuwepo. Matokeo ya akili zetu kutojishughulisha katika ubunifu wa biashara yako wazi tu. Kwa uchache nitaje machache tu.
1. Kwa nini leo ukitafuta biashara za kufundisha kiswahili kwa wageni utakuta Kenya na Uganda wanayo mengi wakati kiswahili ni lugha yetu watanzania?
2. Leo ukitafuta mashirika yanayopandisha watalii wengi mlima Kilimanjaro utakuwa wakenya wanaongoza wakati mlima Kilimanjaro ni wa watanzania?
3. Uliwahi kuchunguza kwa nini wakenya waliweka picha video nyingi kwenye YOUTUBE kumutangaza Babu wa Loliondo alipovuma?
Huu ni baadhi ya ubunifu ambao wenzetu wanaotumia kuanzisha biashara hivyo kufanya kuleta ushindani wa mkubwa wa biashara katika Afrika Mashariki.
Inatupasa tukubali tulipokwama na kuanza kufanya marekebisho makubwa ili tuweze kushindana katika soko huria. Mara zote nawambia wanafunzi wangu kuwa masomo ya ujasiriamali hapa kwetu yameanza miaka michache iliyopita. Hata yale tunayojifunza katika ujasiriamali siyo aliyopaswa kufundisha huyu anayeanza biashara. Masomo mengi ya ujasiriamali ambayo hufundishwa hapa nchini ni kutunza vitabu ya kihasibu, kuandaa michanganuo ya biashara na kutayarisha taarifa za kodi. Kwa mjasiriamali anayeanza haya si sawa kujifunza. Ni vizuri taasisi zote zinazotoa mafunzo ya ujasiriamali zikaanza na kuwaelimisha watu juu umuhimu wa kujua kipaji chako na kukisisimua ili biashara yako itoke huko. Ni vizuri watanzania hawa ambapo madhara ya kumiliki mitaji kwa pamoja bado wanayo wakafundishwa kuwa sasa tumetoka huko sasa tuko kwenye soko huria.(Mind Set).
Sisi katika Elizabethrose Memorial institute tunaamini kuwa jambo la kwanza kabisa kwa mjasiriamali anayeanza nikumweka sawa kiakili ili aachane na yale tayari ambayo alikuwa anaamiki katika kufanya biashara. Tunamjenga kisaikolojia ili aweze kujiamini na kuona kuwa anaweza. Hii inamsaidia kuchangua na kupata malengo yake ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu. Masomo yetu yamegawanika katika sehemu tatu:
1. Business Coaching.
Hii ni kama kocha wa mpira anavyomfundisha mchezaji kucheza mpira. Hufanyika kwa vitengo hasa tukianza na kutambua kipaji cha mhusika na kukitumia katika kuchagua biashara anayoweza kuifanya. Mara nyingi watu huuliza kuwa tunawezaji kupambua vipaji vya watu? Hili tunalifanya pamoja na mhusika kwa kurudi nyuma tangia alipokuwa darasa la kwanza hadi la saba alipenda kufanya nini, na alisifiwa kwa kufanya nini. Kwa kutafakari kwa pamoja mwisho tunajua mtu huyu Mungu alimleta duniani kwa sababu gani.
2. Busness Mentoring.
Hapa tunashughulika na mtu ambaye tayari ameanza biashara lakini anashindwa kukua. Tunachofanya tunamtafutia mtu aliyefanikiwa katika biashara hiyo na kumuunganisha naye ili aweze kuiga wenzake wanafanyaji katika hiyo biashara.
3. Business Consultancy
Hapa ndipo pale tunaangalia biashara kawa ujumla wake; kuanzia kwenye mkakati wa biashara (strategy), malengo na utekelezaji wake na kutoa ushari juu ya maswala ya uhasibu, ukaguzi wa hesabu na maswala ya kodi. Hii ni hatua ya juu ambapo mjasiriamali anakuwa ameshakuwa hivyo kuhitaji huduma hizi.
Naomba hili niliweke sawa, biashara inaweza kuanzishwa katika kipaji chochote. Tunaweza kukusaidia katika eneo lolote kuanzia biashara, michezo, kuigiza, kuimba. Kuwa wale wanaotaka kuonekana hata kwenye luninga tunaweza kufanya kazi na wewe mpaka ukawa celebrity. Tujaribu onone huduma zetu. Na la mwisho ambalo ni tofauti na wengine hatukulipishi ada yoyote mpaka pale utakapoanza kufanikiwa katika biashara yako.Tutafute Tukue Pamoja.
Tunapatikana Ubungo Riverside karibu na kanisa la Father Kwera ukifika pale wewe tuulizie tu.
JCM Marketing Coach ni Taasisi ambayo hutoa mafunzo kwa wafanyabiashara kwa ujumla jinsi ya kuanzisha, kukuza na kuendeleza biashara. Kama umehangaika sana kutafuta biashara ya kufanya, tutabuni pamoja mradi wa kufanya; kama unahangaika sana kutafuta wateja, tuna njia nyepesi na rahisi sana ya kufanya wateja wakutafute wewe. Tunajikita katika Business Coaching, Mentoring na Consultancy.
Tafuta katika Blogu Hii
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni